FORMER TANZANIA MINISTERS MRAMBA AND YONA HAS BEEN GIVEN A CLEANLINESS PUNSHMENT FOR GOVERNMENT FINANCIAL MISS USE>>

By  


Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona wameripoti katika hospitali ya Sinza Palestina na kukabiziwa vifaa kwa ajili ya kufanya usafi.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.

Mawaziri hao, Jul 6, 2015, walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.