#MWANAMKE MUISLAMU ATIMULIWA KWENYE MKUTANO WA TRUMP AMBAYE NI MGOMBEA URAIS MAREKANI#

By  

Donald Trump
Baraza la uhusiano mwema la kiislamu nchini Marekani limemtaka mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, kuomba msamaha kwa kuamrisha mwanamke wa dini ya kislamu kufurushwa kutoka kwa mkutano wake wa kisiasa.
Rose Hamid alilalamikia wito wa bwana Trump wa kuweka marufuku ya muda kwa waislamu wanoingia nchini Marekani.
Wafuasi wa Trump walipoketi, mwanamke huyo alisimama kwa ukimya, huku akivalia vazi lililokuwa na maandishi, salaam. Nimekuja kwa amani.
Wafuasi wa Trump wakimzoma mwanamke wa Muislamu aliyefurushwa katika mkutano wake.
Umati uliyokuwemo ulifanya kelele za kejeli na maafisa wa usalama wakamwondoa.
Bi Hamid mwenye umri wa miaka 56 na ambaye anafanya kazi ya huduma katika kampuni ya moja ya ndege ,baadaye aliamrishwa na afisa mmoja wa usalama kuondoka.
Alizomwa wakati alipokuwa akifurushwa katika mkutano huo.BBC